Romans 5:1-6

Matokeo Ya Kuhesabiwa Haki

1 aKwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, 2 bambaye kwa kupitia kwake tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo ndani yake sasa tunasimama, nasi twafurahia katika tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. 3 cSi hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, 4 dnayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini, 5 ewala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

6 fKwa maana hata tulipokuwa dhaifu, wakati ulipowadia, Al-Masihi alikufa kwa ajili yetu sisi wenye dhambi.
Copyright information for SwhKC